Habari
inayotrend kwa sasa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa ni hii ya
mke wa Donald Trump kudaiwa kuchukua maneno ya hotuba ya mke wa Rais wa
Barack Obama, hotuba hiyo ya Melania inadaiwa kuwa na maandishi
yaliyotolewa kutoka kwenye hotuba ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle,
aliyoitoa miaka minane iliyopita.
Mke
wa Trump amesema alipata usaidizi mdogo sana wakati wa kuandika hotuba
hiyo, ambayo imesisitiza sana maadili ya kifamilia na kujumuishwa kwa
watu wa matabaka yote.
Sehemu moja ya hotuba ya mke wa Trump inasema ……..>>>’Wazazi
wangu walinifunza umuhimu wa kutia bidii kutafuta unachotaka maishani;
kwamba neno lako ndilo linaweka uhusiano na unafaa kutenda unachosema na
kutimiza ahadi kwamba lazima uwaheshimu watu’.
Hotuba ya mke wa Obama mwaka 2008 ilisema: ……>>>’Mimi
na Barack tulilelewa na maadili karibu sawa, kwamba unatia bidii
kutafuta unachotaka maishani; kwamba neno lako linaweka uhusiano na
kwamba unafaa kutenda unachosema utatenda; kwamba lazima uwaheshimu
watu, hata kama huwafahamu, na hata kama haukubaliani nao‘.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni