Kamati kuu ya chama tawala cha
Tanzania,Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemmpendekeza rais John Magufuli
kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Chini ya mwenyekiti wake
aliyekuwa rais wa nchini hiyo Jakaya Kikwete ambaye kikatiba anastahili
kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho hadi mwakani ,Wanakamati 28 kati ya 32 waliofika Dodoma wameidhinisha jina la rais Magufuli kuingoza chama hicho chini ya mwaka mmoja tangu achukue usukani kama rais wa Tanzania.
''Ajenda yetu kuu ni kumpendekeza rais Magufuli kuwa mwenyekiti wetu wa tano wa chama cha mapinduzi'' alisema rais mstaafu Kikwete.
Magufuli ambaye ameongoza kampeini kali dhidi ya ufisadi amekuwa mstari wa mbele wa ''kutumbua majibu hata yale yaliyoko katika chama hicho cha CCM'' na wanadani wa chama wanamtarajia kuendelea kutumbua majibu ya ufisadi ,ubadhirifu wa mali ya umma na uzembe hata katika chama chake.
Takriban wajumbe 1200 wa chama hicho kutoka kote nchini wamekongamana Dodoma kwa mkutano huo wa siku tatu.
Wandani wengi wa chama hicho hawafahamu msimamo wake vyema kwani tangu alipochaguliwa mbunge 1995 Magufuli hakuwahi kushikilia wadhfa wowote chamani hadi pale alipochaguliwa kuwa mgombea wa chama hicho.
Bila shaka uteuzi wake kuwa mgombea wa urais uliibua hisia kali huku viongozi wengi wa chama hicho wengine wenye ushawishi mkubwa wakiondoka chamani na kuhamia katika upinzani.
Katibu mkuu wa chama hicho Abdulhman Kinana anatarajiwa kustaafukwa mujibu wa wandani wa chama hicho ambao hawakutaka kutajwa majina yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni