Adele ametangazwa kuwa mwanamuziki tajiri wa kike nchini Uingereza,kulingana na gazeti la Sunday Times.
Orodha
ya wanamuziki 50 mamilionea nchini Uingereza na Ireland inaonyesha
utajiri wa mwanamuziki huyo kuwa pauni milioni 85 katika nafasi ya 30
ikiwa amejiongezea pauni milioni 35 ikilinganishwa na mwaka uliopita.Mwanamuziki pekee wa kike mwenye utajiri katika orodha hiyo inayoorodhesha taifa la Ireland ni mwanamke wa Ireland Enya mwenye utajiri wa pauni miloni 91.
Kwa mwaka wa tano mfululizo Adele ameorodheshwa katika kilele cha wanamuziki vijana wasio zidi umri wa miaka 30.
Utajiri wa mwanamuziki huyo uliongezeka kufuatia kutolewa kwa albamu ya 25,ikiwa ni yake ya kwanza baada ya miaka minne.
Mwanamuziki huyo aliorodheshwa wa 9 mwaka 2011,lakini ilipofikia mwaka 2012 alikuwa kileleni hadi kufikia sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni