Usiku wa March 10 michuano ya Europa League iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa Barani Ulaya, Uingereza kulikuwa kuna mchezo wa kuvutia zaidi baina yaLiverpool dhidi ya Manchester United katika dimba la Anfield.
Takwimu za vilabu hivi kabla ya mchezo huu kupigwa , Man United alikuwa na takwimu nzuri licha ya kupokea kipigo cha goli 2-0 kwa mujibu wa mechiza mwisho za Manchester United na Livepool walivyokutana, Man United alikuwa kashinda mara nne na Liverpoolmara moja
Hata hivyo takwimu hizo hazikuwa na msaada wowote kwa Man United kwani vijana waJurgen Klopp walifanikiwa kuifunga Man United kuanzia dakika ya 20 kupitia kwaDanny Sturridge kwa mkwaju wa penati, kabla ya dakika ya 73′ Roberto Firminokupachika goli la pili lililoimaliza Man United na kufanya mchezo umalizike kwa Liverpoolkuibuka na ushindi wa goli 2-0.
unaweza kuyatazama hapa magoli ya Liverpool vs Manchester United
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni