Msomi mmoja kutoka
Tanzania Aneth David Mwakilili ni miongoni mwa wasomi wengine
walioteuliwa kuwania tuzo la wanasayansi wachanga barani afrika maarufu
kama The Next Einstein Forum (NEF).
Tuzo hiyo huleta pamoja wasomi
wa sayansi, watunga sheria na washika dau katika seKta mbali mbali
barani afrika, kujadili na kuhimiza sayansi inayoweza kutatua matatizo
yanayokumba bara la Afrika.Washindi wa tuzo hiyo wanapewa ufadhili na usaidizi kutoka kwa wakfu huo ili kutekeleza utafiti wao kikamilifu.
Katika shindano hili Mwakilili, atafanya utafiti ambao utasaidia wakulimu kutokomeza kwekwe na hivyo kuimarisha mazao yao.
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni