Huduma ya WhatsApp
haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya programu
ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1.
Kampuni
ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia
kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016.
Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android.
Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
- Android 2.1 and Android 2.2
- Blackberry OS 7 and earlier
- Blackberry 10
- Nokia S40
- Nokia Symbian S60
- Windows Phone 7.1
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni