YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 18 Novemba 2014

Pale ambapo mastaa wa soka Duniani wanapoamua kupambana na Ebola.

Soka
Kitendo cha mastaa wengi kujitokeza kutoa misaada mbalimbali kwa watu waliopatwa na majanga ama maafa kimekuwa kikitafsiriwa tofauti, ambapo wapo wanaosema mastaa hao wanafanya hivyo kwa ajili ya kujionyesha mbele za watu, lakini wapo wanaoamini kwamba kitendo hicho huonyesha moyo wa kujitolea kusaidia jamii.
Mastaa wa soka Cristiano Ronaldo, Didier Drogba, Neymaar na Gareth Bale ni baadhi ya mastaa ambao wameingia kwenye kampeni za mapambano dhidi ya Ebola.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA ambapo kwenye mtandao wa Youtube zimewekwa video zilizopewa jina la “11 Against Ebola” zinazoonyesha mastaa hao wakitoa elimu kwa madaktari na wataalamu wa afya wanaohudumia waathirika wa Ebola Afrika Magharibi namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads