Hii ndiyo kampuni inayowavalisha Taifa Stars kwa sasa.
Kwa makubaliano hayo TFF walipatiwa vifaa kadhaa vya adidas kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars),Vifaa hivyo ni pamoja na jezi zilizoanza kutumika kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF wanaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni