Hii ndio rekodi nyingine kubwa aliyoiweka Lionel Messi usiku wa jana
Katika mchezo huyo mwanasoka bora wa zamani wa dunia kwa mara nne mfululizo Lionel Messi alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabao 6 ya Barca akifunga mabao mawili, Adriano, na Neymar nao walifunga.
Mabao mawili ya Messi yamemfanya aweke rekodi mpya ya kuwa mwanasoka aliyefunga mabao mengi akiwa kwenye klabu moja katika historia ya soka nchini Hispania.
Messi sasa amemzidi gwiji wa Athletic Bilbao Telmo Zarra ambaye alifunga mabao 333 akiwa na klabu hiyo, Lionel Messi mabao 334 akiwa na kikosi cha Barcelona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni