YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 27 Novemba 2013

JE MGAO KWELI UMEISHAA!?


Siku ya mwisho ambayo ni November 26 2013 si imeshapita? mgao wa umeme je?


umemeNovember 26 2013 ndio ilikua siku ya kumi toka shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutangaza mgao wa siku kumi kwenye baadhi ya mikoa nchini Tanzania ukiwemo 88.5 Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Felchesmi Mramba amezungumza kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema ‘ni kweli kama tulivyotangaza mgao wa Umeme kuchukua siku kumi kutokana na matengenezo yale ya songosongo na kazi imeshakamilika na mgao umekwisha, nataka kuwapa habari hizi njema za furaha watumiaji wa Umeme kwamba adha waliyoipata imefikia mwisho’
millardayo.com : Vipi kama kuna watu bado wataendelea kulalamika kupata mgao wa Umeme?
Mramba : Kama mtu akiona kuna mgao naomba nitoe namba yangu, yeyote atakaeona mgao anipigie 0767 042 009… bado tunatumia mitambo ileile ya Songosongo pamoja na mitambo ya mafuta ya kwetu huku ndio tunatumia, kidogo hali ya maji sio nzuri lakini maji kidogo yaliyopo yanachangia kwa hiyo tukiunganisha nguvu zote hizo na mitambo ya dharura ya mafuta ndio tunapata umeme wa kuwapa Watanzania’

Source: Millardayo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads