Malkia Kassu mshindi wa taji la “Miss Commonwealth Africa” apongezwa na ubalozi wa Tanzania Uingereza
Mtanzania, Malkia Kassu ( wa tatu toka kushoto) akiwa na washindi wenzake – wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi.
Mashindano ya 2013 yalikuwa mjini London Jumamosi Novemba 16 na kwa mara ya kwanza yalikuwa na mshiriki toka Tanzania.Malkia Kassu ( jina la kuzaliwa Mulki Kassu Miraj) alichaguliwa malkia wa Tanzania na bara zima la Afrika.
Wateuzi wa ushindi huo hawakuangalia tu sura, bali tabia, fikra, hamasa na msimamo wa kimaendeleo wa mhusika. Washindani walitoka mataifa mbalimbali duniani.
“Ninataka kuiwakilisha nchi yangu na kuwasaidia wenye maisha magumu, niifanye dunia iwe mahali pazuri zaidi. Nafahamu si kazi rahisi ila nina hakika kila mmoja wetu akijumuika na mwenzake mabadiliko mema zaidi yatafanyika. Tanzania ni nchi ya amani na ninaamini amani na mapenzi vyaweza kuongezeka katika jumuiya zetu.” – Kassu
Kutoka kushoto ni mdhamini, Ali Sungura,
Balozi wetu Uingereza , mheshimiwa Peter Kallaghe, sahiba mkuu Aisha
Mohammed na Afisa Ubalozi, Allen Kuzilwa
Malkia Kassu
Malkia Kassu akipongezwa na marafiki, Andrew Matt na Aisha Mohammed.
Malkia Kassu akiwa na mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Diamond karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni