Unataka kujua Mabilionea wa Afrika waliotajwa kwenye list mpya? huyu Mwanamke nae katisha
Imefahamika kwamba bara la Afrika lina mabilionea wengi sasa hivi kuliko ilivyokua ikifikiriwa ambapo hii imefahamika baada ya jarida la Ventures kuripoti kuwa pamoja na idadi ya mabilionea kuzidi kuongezeka bado asilimia kubwa ya Waafrika ni masikini wa kutupwa.
Kabla ya hii ripoti, idadi ya mabilionea wa Afrika ilikuwa 16 lakini imeongezeka na kufikia 55 na jarida hili limeweza kuwagundua
mabilionea wengi kwa kuchunguza kwa siri ili kuepuka baadhi yao ambao
ambao wanaficha taarifa za utajiri wao, yani huwa hawapendi kuzitoa kwa
wanahabari.
kati ya mabilionea hao 55, 20 wanatokea Nigeria na wanajumuisha wafanyabiashara wa mafuta huku Afrika kusini na Misri zikiwa na mabilionea tisa ambapo alietajwa kuwa ni tajiri kuliko wote Afrika ni Mnigeria Dangote ambae ana utajiri wa dola bilioni 20.2
Dangote
alitengeneza utajiri wake kupitia biashara ya saruji na hadi leo
anaongoza kampuni ambayo inahusika na biashara za unga wa kupikia,
sukari pamoja na mafuta.
Mwanamke tajiri kuliko wote Afrika anatokea Nigeria pia ambaye Folorunsho Alakija ambae kampuni yake ya fama oil inamilki visima vya mafuta ambavyo alivipata mwaka 1993, alianza kama mwanafunzi wa masuala ya mitindo huko London na alikuwa akibuni mavazi ya rais wa zamani wa Nigeria Ibrahim Babangida.
Tajiri
toka afrika kusini Nicky Oppenheimer ana utajiri wa dola bilioni 6.5
utajiri ambao ulipatikana kwenye madini hususan madini ya almasi ambayo
amerithi toka kwa familia yake.Pamoja na hii ripoti kunifikia bado haijanipa mabilionea wengine waliobaki wanatoka nchi gani… naendelea kufatilia
Source:Millardayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni