William alikuwepo London hapo jana ambapo inaaminika amefanyiwa vipimo vya afya kabla ya uthibitisho wa usajili wake huku Lamela yeye akitarajiwa kutua jijini humo hii leo .
Hadi sasa Spurs imeshatumia zaidi ya pundi milioni 50 kuwasajili Roberto Soldado ,Nacer Chadli,Paulinho na Etienne Capoue na usajili wa Willian pamoja na Lamela utaigharimu Spurs jumla ya paundi milioni 60.
Willian ambaye ni raia wa Brazil alianzai soka lake ndani ya klabu ya Shakhtar Donetsk ambako alijijengea jina akiwa na Wabrazil wenzie kama Fernandinho na Alex Texeira kabla hajajiunga na Anzhi Makhachkhala .
Erik Lamela amekuwa akiichezea klabu ya As Roma ambayo imemsajili toka Argentina ambapo inaaminika kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi wa Spurs Branco Baldini ambaye aliwahi kuwa na nafasi hiyo ndani ya klabu ya As Roma amekuwa sehemu muhimu sana ya mchezaji huyo kuja Tottenham.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni