Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt hapo jana alitwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya dunia ya mchezo wa riadha yanayoendelea nchini Urusi .
Bolt alitwaa medali hiyo baada ya kumaliza mbio hizo ndani ya muda wa sekunde 9.77 ambapo alimaliza mbele ya wakimbiaji toka Marekani na Jamaica ambao ni Justin Gaitlin na Nestor Carter.
Ubingwa huu ni wa kwanza kwa Bolt tangu mwaka 2009 wakati alipotwaa ubingwa huo kwa mara yake ya kwanza . Bolt alishindwa kutetea ubingwa wake kwa mashindano ya mwaka 2011 baada ya kuondolewa kwenye mbio za mia 100 kutokana na kuanza kala ya wenzie ambapo ubingwa huo ulikwenda kwa Mjamaica Mwenzie Yohan Blake .
Blake kwa bahati mbaya alishindwa kutetea taji lake kwa mashindano ya mwaka huu baada ya kuumia mazoezini .
Wakimbiaji wawili Asafa Powell toka Jamaica na Tyson Gay wameyakosa mashindano hayo baada ya kugundulika wanatumia dawa zilizopigwa marufuku wiki chache kabla ya mashindano kuanza .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni