YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 2 Agosti 2013

Oloya atua Dar, asaini Yanga miaka miwili- Tanzania

HATIMAYE Yanga imefanikiwa kuinasa saini
ya kiungo raia wa Uganda, Moses Oloya
(pichani) , baada ya kumsainisha mkataba
wa miaka miwili , jana jijini Dar es Salaam.
Oloya awali alikuwa akiwaniwa na Simba
waliotangulia kuanza mazungumzo na
nyota huyo , lakini ilishindikana kutokana
na kuwa na mkataba na Klabu ya Saigon
Xuan Thanh ya Vietnam .
Taarifa za kuaminika zilizolifikia Championi
Ijumaa , zimesema kuwa Oloya alitua jijini
Dar es Salaam, juzi usiku kwa siri , majira
ya saa nne akitokea Vietnam kupitia nchini
Kenya, ambapo mara baada ya kutua
alipelekwa moja kwa moja katika hoteli
moja kubwa jijini (jina tunalo ) na kufichwa
humo.
Baada ya kufika hotelini hapo , wahusika
walipewa maelekezo kuwa hawatakiwi
kutoa taarifa zozote juu ya mchezaji huyo
ambaye alikuwa akisubiri kusaini.
Jana mchana , alikutana na viongozi wanne
wa juu wa Yanga, ambao walizungumza
kwa kirefu na nyota huyo , mwisho
wakakubaliana kila kitu juu ya mkataba
ambapo Oloya alisaini mkataba wa miaka
miwili ulioigharimu klabu hiyo zaidi ya
dola 74 ,000 (Sh milioni 120).
“Kila kitu tumekuwa tukikifanya kwa siri
kubwa, hatukutaka kuanza kuzungumza
kama wanavyofanya wenzetu ( Simba) ,
tulikuwa na uhakika kuwa huyu mchezaji
(Oloya) tutamleta hapa Yanga, tunashukuru
hilo kukamilika, sasa tutakwenda kumalizia
vitu vidogo sana ,” alisema kiongozi mmoja
wa Yanga na kuongeza:
“Tumelazimika kufanya hivi kwa kuwa
tulitaka kila kitu kimalizike kabla ya
kufungwa kwa dirisha la usajili, sasa
tunageuka katika kazi ndogo iliyosalia ya
kumalizana na klabu yake ambayo
amebakiza muda wa wiki zisizozidi tatu
katika mkataba wake .”
Kufuatia kukamilika kwa usajili huo, nyota
huyo aliondoka jana usiku akiongozana na
mmoja wa mabosi wa klabu hiyo (jina
tunalo) tayari kwenda kumalizana na klabu
yake ya nchini Vietnam kabla ya kurudi
kuja kuitumikia Yanga.
Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuandika juu
ya Yanga kufanya mazungumzo na Oloya,
baada ya Simba kusema kuwa inamuwania
Mganda huyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads