YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 27 Agosti 2013

HII NI NOMA, WANAFUNZI NCHINI LIBERIA WAFELI WOTE MTIHANI WA KUJIUNGA NA CHUO. HAKUNA ATAYEJIUNGA NA CHUO. SOMA HAPA

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia,
wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa
mwisho wasekondari na hivyo kumaanisha
kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu
kuingia chuo kikuu.
Waziri wa elimu wa Liberia amesema
ameshinda kufahamu ni kwa nini hakuna
wanafunzi hao wamefeli kiasi hicho.
Zaidi ya wanafunzi elfu ishirini na watano
walianguka mtihani huo ambao ungewapa
fursa ya kujiunga na chuo kikuu cha Liberia
ambacho ni moja ya vyuo vikuu
vinavyoendesha na serikali.
Lakini wasimamizi wa chuo hicho wameiambia
BBC kuwa wanafunzi hao hawakuwa makini na
ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza ambayo
ilitumiwa kuwatahini.
Taifa la Liberia linaendelea kujinasua kutokana
na athari za mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe yaliyomalizika zaidi ya miaka kumi
iliyopita.
Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye
pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel,
amekiri kuwa mfumo wa elimu nchini humo
bado ungali duni na unahitaji marekebisho ya
dharura.
Mwandishi wa BBC mjini Monrovia, anasema
shule nyingi nchini humo havina vifaa vya
kimsingi na waalimu waliohitimu.
Lakini hii ni mara ya kwanza katika historia ya
taifa hilo kwa wanafunzi wote kufeli mtihani
huo licha ya kulipa ada ya usajili ya dola
ishirini na tano.
Chuo hicho kikuu ambacho kina idadi kubwa
ya wanafunzi hakitakuwa na wanafunzi wa
mwaka wa kwanza wakati muhula mpya
utakapoanza mwezi ujao.
Lakini wanafunzi wengi wanasema hawajaamini
matokeo ya mtihani huo na waziri wa Elimu
Etmonia David-Tarpeh, ameiambia BBC kuwa
anatarajia kukutana na wasimamizi wa chuo
hicho ili kujadili suala hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads