Msajili wa vyama vya siasa nchini , John
Tendwa .
Hatimaye msajili wa vyama vya siasa
nchini, John Tendwa ameibuka na kusema
sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama
kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari
muda mfupi uliopita Tendwa amesema
CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha
mgambo ambacho ni kinyume na sheria ,
katiba ya nchi na sheria za usajili wa
vyama.
Msajili huyo amesema kwamba kama
madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi
cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa
CCM madai hayo hayana msingi wowote
kwani kama CHADEMA wana taarifa
kwamba Green Guard wanahatarisha amani
basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili
lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.
Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi
wake ni wa mwisho na atakapoifuta
CHADEMA maamuzi yake hayapingwi
popote kisheria.
Source: Globalpublishers
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni