Liu Fenghe akiwa hospitali na chuma
kichwani .
Picha ya X -ray ikionyesha jinsi chuma
hicho kilivyoingia kichwani mwa bwana
Liu . ( Picha: HAP/ Quirky China News/
Rex)
FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini
China, amenusurika kifo baada ya
kuchomwa na chuma kichwani na kuzama
inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita 20 .
Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa
bahati mbaya alidondokewa na chuma
hicho kilichomchoma kichwani.
Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema :
"Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote
Liu alikuwa katika dimbwi la damu. "
Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka
kutoka ghorofa ya 25 ya jengo
walilokuwemo mafundi hao mpaka
kusababisha maafa hayo .
Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka
katika hospitali iliyopo jimbo la Shanghe
nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo
tena katika hatari japo bado haijajulikana
ni lini ataweza kurudi kazini .
Translate
Jumanne, 16 Julai 2013
ANUSURIKI KIFO BAADA YA KUCHOMWA NA CHUMA SENTIMITA 20 KICHWANI
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni