YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 21 Juni 2013

MWANAFUNZI APIGWA RISASI TUMBONI CHUO KIKUU CHA UDSM USIKU WA KUAMKIA LEO

Taarifa zilizonifikia katika chumba cha habari
zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo
kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la
Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi
usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo
chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa
mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo
walikuwa wanajisomea na kuandaa
“Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na
watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao
na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha
habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao
walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za
fedha, na majambazi kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate
hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo
mmoja wao akaamua kuwafuata na
kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi
huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini
na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa
kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi
wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili
kupata gari ili wamkimbize mwenzao
Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa
hakuna majibu na ndipo walipoamua
kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi.
Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa
Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka
sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa
FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo
ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa
chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka
serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo
vya kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia
katika mtandao huu amboa umefunga safari ya
kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia
nini kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi
wa hadharani katika shule za Chuo hicho
ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa
wakiporwa komputa zao mchana kweupe
maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya
uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma
(SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na
kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads