YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 18 Juni 2013

Mbunge ataka Kiswahili kitumike hadi vyuo vikuu

MBUNGE wa Karagwe, Gosbert Blandes
(CCM), amehoji lini serikali itapitisha
Kiswahili kitumike kuanzia Shule za Msingi
hadi Vyuo Vikuu. Aidha, alisema mwaka
2004, Umoja wa Afrika ulipitisha Kiswahili
kiwe ni lugha ambayo itatumika katika
mikutano na shughuli mbalimbali.
“Je, serikali imejiandaa vipi kupeleka
wakalimani wa kutosha kutoka Tanzania ili
waweze kujipatia ajira?” alihoji.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Amos Makala alisema jitihada zinafanywa
na taasisi hizo za kukuza Kiswahili
mojawapo kuandika vitabu vingi vya
kufundishia na kuongeza wataalamu.
“Nasema wazo hilo tumelipokea na sisi
ndani ya serikali tunaendelea kulifanyia
kazi na hata wakati tunawasilisha bajeti
yetu zilitoka hoja hizo za kuwa Kiswahili
kifundishwe madarasani,” alisema.
Aidha, Makala alikiri kupitishwa kwa
azimio hilo na kuongeza kuwa:
“Kama Tanzania tumeona kuwa hii ni fursa
muhimu na tayari moja ya kazi
zinazofanywa na Taasisi za kukuza
Kiswahili, BAKITA, BAKIZA ni kuongeza
wataalamu zaidi ili waweze kupata ajira
hiyo.”
Aliongeza kuwa Tanzania kama Tanzania
mjini Addis Ababa kuna kituo cha
kufundishia lugha ya Kiswahili. Awali katika
swali la msingi, Mbunge wa Tarime,
Nyambari Nyangwine (CCM) alitaka
kufahamu kama nchini Tanzania kuna Sera
ya Lugha.
Pia, alihoji kama ipo, je, sera hiyo ya
Lugha imeipatia hadhi gani lugha ya
Kiswahili.
Aidha, alitaka kujua kuna mkakati gani
mahsusi wa kuifanya Lugha ya Kiswahili
kuwa ya kufundishia kwa viwango vyote
vya elimu hapa nchini.
Akijibu swali hilo, Makala alisema Tanzania
hakuna andiko mahususi au linalosimama
pekee kama Sera ya Lugha, bali suala la
lugha limezingatiwa kama Sura maalumu
muhimu ndani ya Sera ya Utamaduni ya
mwaka 1997.
Alisema katika andiko hilo la sera ya
Utamaduni, Kiswahili kimetambuliwa kuwa
siyo tu lugha ya mawasiliano mapana
nchini bali pia ni lugha ya taifa na
mojawapo ya lugha rasmi mbili za Taifa.
Aidha, alisema miongoni mwa mikakati
mahsusi ya kuifanya lugha ya Kiswahili
kuwa lugha ya kufundishia ni jitihada
zinazoendelea za wataalamu wa Asasi za
ukuzaji wa Kiswahili nchini ambazo ni
kuboresha sarufi ya Kiswahili, kutunga
Kamusi za Kiswahili za masomo na taaluma
mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads