YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 7 Juni 2013

Kutana na Mtoto wa kitanzania anayetengeneza Application za simu na kuwauzia Nokia.

Alvin Walter Makundi ni kijana mdogo wa
Kitanzania anayeishi na wazazi wake nchini
Singapore. Akiwa na umri wa miaka 14 na
mwanafunzi wa kidato cha pili huko
Singapore, tayari ameshatumbukiza jina lake
katika orodha ya wataalamu wa application
katika moja ya makampuni makubwa duniani
ya kutengeneza simu za mkononi ya NOKIA,
ambapo anatengeneza applications ambazo
anazituma katika kampuni hiyo ambayo nayo
bila hiana huitumia. Kwa idhini ya mama yake.
Globu ya Jamii ilipata fursa ya kuongea naye
kuhusu hayo maajabu anayoyafanya. Msikilize.
hapo chini...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
Bw. Walter P. Makundi, ambaye ni Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Watanzania waishio Singapore
siku alipokutana na kuzungumza nao. Bw.
Makundi, ambaye ni Meneja mradi wa
kampuni kubwa ya ujenzi ya APCO PTE LTD ya
hapo Singapore, ndiye baba mzazi wa Alvin.
Kulia kwake ni mkewe, Mama Alvin.
Chini Rais Kikwete akisalimiana na Alvin
ambaye aliongozana na mama yake pamoja na
dada kuja kumuaga wakati Rais akiondoka
Singapore usiku huu.
MTIZAME HAPA

http://www.youtube.com/watch?v=bcBxmfTz2qg&feature=youtube_gdata_player

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads