YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 11 Juni 2013

BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA ADAI KUWA UJIO WA RAIS OBAMA SI KWA AJILI YA RASILIMALI ZA MTANZANIA

Akiongea na waandishi wa habari jana,
Balozi wa Marekani nchini Tanzania,
Alfonso Lenhard amesema ziara ya mwezi
ujao ya Rais wa Taifa la Marekani, Barack
Obama nchini Tanzania haina ajenda ya
siri: "kuna maswali mengi naulizwa kwa
nini Rais Obama amechagua kuzuru
Tanzania? Ni kweli Rais wetu anakuja
malengo ya ziara yake yatajikita katika
mambo ambayo ni malengo ya Marekani
kwa Afrika, ambayo ni uhusiano wa
kiuchumi, kuimarisha demokrasia na
kuwekeza katika kujenga kizazi kijacho
cha uongozi."
Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi
wa habari kuhusu uhusiano wa ujio wa
Rais Obama na rasilimali za Tanzania,
Balozi Lenhardt alisema: "Ni
kweli Obama atakuja Tanzania. Lakini
niwahakikishie tu kuwa haji kupora
rasilimali za Tanzania, kwani Marekani
ina rasilimali nyingi zinazojitosheleza..."
“Watanzania ni watu wapole na
wakarimu ila mna tatizo moja la kuhofia
kila jambo. Kila kitu mnachofanyiwa
mnaona kuna baya linakuja. Sisi tuna nia
njema ya kuwasaidia kuendelea.”
Akizitaja sababu nne zilizosababisha Rais
Obama kuichagua Tanzania, Lenhardt
alisema:

1. Tanzania ni nchi pekee kati ya nchi
tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), ambayo Obama
amechagua kufanya ziara yake ya
kikazi kutokana na kuwa mfano wa
utawala bora, demokrasia na
ushirikishaji wa watu wake wakati wa
kufanya uamuzi unaogusa maisha yao
ya kila siku. Akasema Tanzania ni nchi
ya mfano linapokuja suala la uongozi
bora na ndiyo maana imekuwa na
amani na utulivu kwa muda mrefu
ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini
mwa Jangwa la Sahara: “Nchi nyingi za
Afrika zinazoizunguka Tanzania
zimekuwa na matatizo ya vita vya
wenyewe na hata ukosefu wa utawala
bora,” alisema Balozi Lenhardt ingawa
alidokeza kuwa katika siku za karibuni
imekuwa ikikabiliwa na changamoto
mbalimbali kutokana na matukio ya
uvunjifu wa amani.

2. Jitihada za Serikali ya Marekani
kutengeneza mazingira mazuri ya
uwekezaji na kasi ya ukuaji wa
uchumi: “Rais Obama anakuja kuunga
mkono juhudi za Watanzania katika
kutengeneza mazuri ya uwekezaji lakini
bila kusahau kuwa kasi ya ukuaji wa
uchumi wa Tanzania imeivutia Serikali
ya Marekani.”

3. Kuisaidia Tanzania kuendeleza fursa
mbalimbali za kujiletea
maendeleo. Alisema uendelezaji huo wa
fursa una lengo la kuisaidia Serikali ya
Tanzania kukabiliana na tatizo la
umaskini na kwamba Marekani ni moja
ya nchi zinazoongoza kwa kutoa fedha
nyingi za misaada na akisema kwa
mfano, mwaka 2012 pekee ilitoa Dola
750 milioni. Aidha, alisema nchi yake
imekuwa ikitoa misaada mingi kupitia
Shirika la Millenium Challenge (MCC),
ambayo imejikita zaidi katika kusaidia
sekta za umeme, maji na
miundombinu. Alisema Tanzania
inaunga mkono jitihada za Serikali
kujitosheleza kwa chakula na inafadhili
Mkakati wa Kukuza Kilimo Kusini mwa
Tanzania (SAGCOT): “Tunaunga mkono
mpango wa SAGCOT kupitia Mfuko wa
Rais wa Marekani unaoitwa `Feed the
Future’ lengo likiwa kuifanya Tanzania
kupiga hatua katika kilimo,” alisema
balozi huyo.

4. Kuhimiza haja ya Afrika kutayarisha
viongozi wa kizazi kijacho. Ameanzisha
programu ya kuandaa viongozi wa
kizazi inayoitwa `Young African
Leaders Initiative’ na Watanzania
watatu, Modesta Lilian Mahiga, Masoud
Salim Mohamed na Malula Hassan
Nkanyemka walishiriki katika mpango
huo na kukutana na kiongozi huyo
mwaka 2010: “Rais Obama anataka
kusaidia kuandaa viongozi wa kizazi
kijacho wa Afrika kusimamia vizuri
rasilimali za nchi,” alisema.
"Tunaweza tusitoe taarifa za kina juu ya
ziara hii, kwani mambo yote yanaratibiwa
na Ikulu ya Marekani, lakini niseme
kwamba sisi tunahitaji kuwa na marafiki
na Tanzania ni rafiki yetu na sio suala la
kuchukua rasilimali zenu..."
"Hatuna ajenda ya siri juu ya ziara hiyo.
Ila kampuni za Marekani zimekubali kuja
nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za
kuwekeza na lazima zitafuata taratibu
zote..." alisema Lenhardt na kuongeza
kuwa akiwa nchini, Obama atakutana na
viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na
asasi zisizo kuwa za kiserikali ambazo ni
muhimu katika ustawi wa nchi hasa
katika maeneo tajwa hapo juu, alisisitiza
Balozi huyo.
USHINDANI NA CHINA
Rais wa China, Xi Jinping aliitembelea
Tanzania Machi mwaka huu na ujio wa
Obama umetafsiriwa na baadhi ya watu
kuwa ni ushindani wa mataifa hayo
mawili katika kusaka na kunufaika na
rasilimali za Afrika.
Akizungumzia ushindani na China
kuhusiana na fursa za kuwekeza na
kuvuna rasilimali za Afrika, Balozi
Leinhardt alisema imani yao ni kuwa
China inadumisha urafiki na Tanzania kwa
nia ya kuisaidia kuendelea... “Sisi hatuna
shida na China, kwani tunaamini wako
kwa ajili ya kusaidia. Ilimradi tu wawe na
dhamira safi katika kuwasaidia.”
Nchi nyingine atakazozuru Rais Obama ni
Senegal na Afrika Kusini. Ataanza ziara ya
kutembelea nchi hizo tatu Juni 26 — Julai
2, 2013.
Katika safari hiyo, Obama atafuatana na
mkewe, Michele na wanawe, Sasha na
Malia. Atakuwa Rais wa tatu wa Marekani
kuitembelea Tanzania baada ya Bill Clinton
mwaka 2000 na George Bush mwaka 2008.

http://www.youtube.com/watch?v=9vThaHXoBnc&feature=youtube_gdata_player

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads