YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 7 Juni 2013

AIRTEL YAONGEZA MUDA VIFURUSHI VYA AIRTEL YATOSHA, SASA HUDUMA MASAA 25 KWA SIKU===>>Soma haPa..

Dar es Salaam Juni 5 2013 : Airtel
Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yao
ya kuwapatia wateja wake unafuu zaidi
kupitia huduma yake ya AIRTEL YATOSHA
nchini ambapo sasa wateja watafurahia
Vifurushi vya Airtel Yatosha kwa masaa 25
kwa siku, hii itawawezesha watanzania
kufurahia kupiga simu mtandao wowote
kwa gharama nafuu kwa muda mrefu zaidi .
Akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel
yatosha masaa 25 Meneja Uhusiano wa
Airtel Jackson Mmbando alisema” kuanzia
sasa, huduma ya Airtel yatosha kwa siku
itakua kwa masaaa 25 kuanzia pale mteja
anapojiunga na huduma, yaani masaa 24
ya kuongea na kama vile haitoshi Airtel
yatosha inakuongezea saa jingine moja la
ziada . Sasa wateja wa Airtel watafurahi
kupiga simu kwa gharama nafuu na kwa
muda zaidi kuliko ilivyokuwa awali ”.
“Hii ni ya kwanza na pekee kutoka Airtel,
Airtel yatosha itaendelea kuwa suluhisho la
mawasiliano ya huduma za simu kwa
watuamiaji na wateja wa Airtel nchi nzima
” aliongeza Mmbando
Airtel yatosha ni huduma iliyoanzishwa ili
kuleta kuvunja mipaka kwa watanzania na
kuwawezesha kuwasiliana ndani na nje ya
mtandaa kwa gharama nafuu. Kujiunga na
huduma hii piga * 149* 99# na atapata
majibu papo hapo achague unataka
Yatosha WIKI au Yatosha SIKU au Tosha ya
Mwezi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads