MWENYEKITI wa
Chama cha
Demokrasia na
Maendeleo
(Chadema), Freeman
Mbowe, amemshitaki
kwa wanachama wa
chama hicho, Spika
wa Bunge, Anne Makinda. Akizungumza
na wanachama hao katika Ukumbi wa
Vijana uitwao Wajenzi mjini hapa jana,
Mbowe alitumia muda mwingi
kumchambua Spika Makinda na kusema
kuwa anatumika kuwadhoofisha wabunge
wa upinzani.
Mkutano huo pia ulifanyika kama sehemu
ya maandalizi ya uzinduzi wa Kanda ya
Kati ya chama hicho, inayohusisha Mikoa
ya Morogoro, Singida na Dodoma.
Katika mkutano huo, Mbowe ambaye pia
ni Mbunge wa Hai, alitumia muda mwingi
kukichambua kitabu cha Kanuni za Bunge
ili kuwadhihirishia wanachama hao ukweli
wa uonevu wa Spika dhidi ya chama
chake.
“Kwa sasa CCM wanatumia muda mwingi
sana kuwapotosha wananchi, kwamba
wabunge wa Chadema hawajui Kanuni za
Bunge.
“Nawaambia kanuni tunazijua, tunazo na
kila mmoja anajua zilitungwa enzi za
mfumo wa chama kimoja, japokuwa hadi
sasa bado zinatumika.
“Hata zinapofanyiwa marekebisho, CCM
wamekuwa wakitumia nguvu kuweka
vipengele vinavyowabeba, hilo tunalijua.
Kwa hiyo, mtaona kwamba, wakati akina
Lissu (Tundu Lissu, Mbunge wa Singida
Mashariki), walipofukuzwa bungeni na
wenzake, Naibu Spika alikiuka kanuni
makusudi.
“Kanuni ya pili, kifungu cha pili
alichotumia Naibu Spika hakikutumika
ipasavyo, kwani kanuni hiyo inatumika
katika jambo ambalo limetokea bungeni
wakati halizungumzwi kwenye kanuni.
“Jambo la wabunge kutotii kiti cha Spika
lina kanuni zake, kwa hiyo, Naibu Spika
alitakiwa kutumia kanuni ya 74 ambayo
ilikuwa ikimtaka apeleke suala hilo katika
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge, ili waliokaidi kiti cha Spika
wakajieleze huko.
“Lakini kwa utashi wake, aliamua
kupindisha kanuni kisha akatetewa na
Spika mwenyewe, ambaye anajifanya
mcha Mungu wakati siyo kweli,” alisema
Mbowe.
Pamoja na hayo, aliwataka wanachama
wa chama hicho kutobweteka na
umaarufu wa chama chao, badala yake
wafanye kazi kwa bidii ili wafanikiwe
kuiondoa CCM madarakani wakati wa
uchaguzi mkuu 2015.
Pia, alikemea vitendo vya rushwa ndani
ya chama hicho na kwamba mgombea
atakayetoa rushwa kwa wanachama ili
achaguliwe, atachukuliwa hatua za
kinidhamu.
Awali, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Wilbrod Slaa, naye alimshutumu Spika
Makinda na kusema uamuzi anaotoa
bungeni hautoi kwa ridhaa yake, bali kwa
maagizo ya Serikali.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka wabunge
wa Chadema, kutokata tama, bali
waendelee kupambana kisiasa kama
zinavyopambana katika soka Timu za Soka
za Real Madrid na Barcelona.
Translate
Jumapili, 21 Aprili 2013
Chadema wamshitaki Makinda
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni