Vipuli viwili vya
almasi, vimevunja rekodi ya dunia kwa kuuzwa kwa kiwango kikubwa zaidi
cha pesa, cha takriban dola milioni 58, katika soko la mnada nchini
Uswizi.
Vipuli hivyo viko sawa, lakini kimoja kina rangi ya waridi na chengine ni cha buluu.Viliuzwa tofauti tofauti lakini vikanunuliwa na mnunuzi mmoja.
Kulikuwa na wasiwasi kwamba vipuli hivyo, vinavyojulikana kama Apollo na Artemis havitakuwa pamoja baada ya kupigwa mnada mjini Geneva.
- Mhubiri apata almasi ya mamilioni ya dola Sierra Leone
- Almasi isio ya kawaida yaweka rekodi mpya katika mnada
- Grace Mugabe katika mzozo wa pete ghali ya almasi
Hata ijapkuwa ziliuzwa tofauti lakini vitasalia kuwa pamoja baada ya kupata mnunuzi mmoja.
Alamasi ya Apollo yenye rangi ya buluu iliuzwa kwa takriban dola milioni 42 huku Artemis yenye rangi ya waridi ikiuzwa kwa dola milioni 15.5
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni