Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe amesafiri kwenda Singapore kufanyiwa uchunguzi wa
kimatibabu, gazeti la serikali la Herald limeripoti.
Kiongozi huyo
wa umri wa juu zaidi duniani, ambaye amekuwa akionekana dhaifu
hadharani siku za karibuni, alihutubia wajumbe katika mkutano mkuu wa
Baraza la uchumi Duniani Afrika Kusini wiki iliyopita.Shirika la habari la AFP linasema alihutubu "kwa sauti hafifu huku akiwa amejibwaga kwenye kiti".
Gazeti la Herald linasema amekwenda Singapore kwa "uchunguzi wake wa kawaida wa kimatibabu".
Bw Mugabe anatarajiwa kurejea nyumbani kwa wakati kuweza kuhudhuria mazishi ya jaji mkuu wa zamani Godfrey Chidyausiku.
- Mugabe: Upinzani hauninyimi usingizi
- Mugabe: ''Nilikufa kisha nikafufuka''
- Aliyetabiri kifo cha Mugabe akamatwa Zimbabwe
Licha ya umri wake, chama tawala cha Zanu-PF kilimuidhinisha Bw Mugabe kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika mkutano Februari, mkewe, Grace Mugabe, alisema: "Siku moja Mungu atakapoamua kwamba Mugabe afe, basi tutakuwa na maiti yake kama mgombea kwenye karatasi ya kura."
Source:BBCSwahili
Bw Mugabe ameongoza taifa hilo tangu uhuru mwaka 1980.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni