Aliyekuwa rais wa
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuhudumu katika baraza kuu la
wakimbizi duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi
wanaolenga kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.
Kulingana
na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, taarifa kwa vyombo vya habari
ilimtaja Bwana Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo
chini ya uenyekiti wa waziri wa maswala ya kigeni nchini Canada Lloyd
Axworthy.Gazeti hilo limesema kuwa Hina Jinali kutoka Pakistan na Rita Sussmith kutoka Ujerumani watafanya kazi pamoja na bwana Kikwete kama wenyekiti wenza huku Paul Heinbecker akichaguliwa kama naibu huku naye Fen Hamson akihudumu kama mkurugenzi.
- Rais Magufuli amteua Salma Kikwete
- Kikwete: Naomba niachwe nipumzike
- Magufuli: Mwacheni Kikwete apumzike
Baraza hilo litaleta mabadiliko ili kusaidia kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kimataifa kwa wakimbizi unaeleweka, unafanyika kwa njia ya usawa na haki, ilisema taarifa hiyo.
Baraza hilo pia litashirikisha madiwani 17 wa mabaraza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni