YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 17 Mei 2017

Kenya: Maafisa wa Kamati ya Olimpiki washtakiwa kwa wizi

Baadhi ya wasimamizi wa kamati ya Olimpiki
Maafisa wa kamati ya Olimpiki NOCK wanakabiliwa na mashtaka ya usimamizi mbaya wa fedha
 
Wasimamizi wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya, NOCK, wameshtakiwa kwa njama za wizi na usimamizi mbaya wa fedha na sare za kikosi cha Kenya katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika mjini Rio , Brazil mwaka uliopita.
Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya, ODPP imetangaza kuwa, baada ya kutathmini uchunguzi, maafisa hao wanastahili kushtakiwa kwa makosa hayo.
Wasimamizi hao wakiwemo msimamizi wa timu ya Kenya kwenye Olimpiki, Stephen Soi, aliyekuwa naibu mkuu wa ujumbe wa Olimpiki, Bernard Ekumbo, katibu mkuu, FK Paul na naibu meneja wa timu hiyo, Pius Ochieng watafikishwa mahakamani baadaye mwezi huu kujua hatma yao.
Rio 2016: Kamati ya Olimpiki Kenya yavunjiliwa mbali
Mwaka uliopita, maafisa wa polisi walinasa sare za wanariadha katika makazi ya naibu mwenyekiti, Ben Ekumbo kufuatia malalamiko ya wanariadha kuwa hawakupokea sare za kutosha.
Aidha, baadhi ya maafisa wengine wa kikosi cha Kenya kwenye Olimpiki, walieleza kudhalilishwa katika mashindano hayo kwa kutopewa makazi mjini Rio na kuishi katika hali duni.
Kikosi cha Kenya kilikumbwa na sakata mbalimbali licha ya kuandikisha matokeo mazuri kwenye mashindano ya Olimpiki.
Wanariadha wa Kenya waishi 'mtaa wa mabanda' Rio
Licha ya changamoto hizo, wanariadha wa Kenya walifanya vyema na kuondoka na medali 6 za dhahabu, 6 za fedha na moja ya shaba na kuandikisha matokeo bora zaidi ya Kenya kwenye Olimpiki.
Kesi dhidi ya wanne hao itasikizwa tarehe 31 mwezi huu kabla ya kuendelea tena tarehe 26 mwezi ujao wa Juni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads