Rais mpya wa FIFA
Gianni Infantino amefungua afisi ya shirikisho la kandanda la Sudan
Kusini katika safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu achaguliwe rais
wa shirikisho hilo la soka duniani mwezi uliopita.
Infantino alilakiwa kwa shangwe na vigelegele na wenyeji wake.Aidha Infantino alitumia ziara hiyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Rais huyo wa FIFA ameratibiwa kufanya mkutano na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir mjini Juba kabla ya kushuhudia mechi ya kuwania kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika kati ya Sudan Kusini na Benin.
Kama ilivyoada alivishwa mavazi ya kitamaduni na wenyeji wake.
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni