YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 26 Julai 2013

TAIFA STARS KUSHAMBULIA MWANZO MWISHO KESHO

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye
mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu ) dhidi
ya Uganda kuwania kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa
Wachezaji wa Ndani ( CHAN) zitakazofanyika
mwakani nchini Afrika Kusini ni
kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.
Kocha Kim Poulsen amesema maandalizi ya
Taifa Stars jijini Mwanza kwa ajili ya mechi
hiyo ambayo Uganda inaongoza kwa bao
1- 0 yalikuwa mazuri , lakini mabao ni
muhimu hivyo watashambulia bila kusahau
kulinda lango lao.
“Unapocheza mechi za aina hii za
nyumbani na ugenini , huku mwenyeji
akiwa anaongoza mabao yana maana
kubwa katika mechi . Mabao yanabadili
mchezo na pia wachezaji kifikra ,” amesema
Kim akizungumza na waandishi wa habari
kwenye hoteli ya Mt. Zion ambayo Stars
imefikia.
Amesema katika mechi ya kwanza
walitengeneza nafasi nyingi lakini
hawakuzitumia, hivyo wamekuwa wakifanya
mazoezi ya kushambulia, jinsi ya
kutengeneza nafasi, na jinsi ya kumalizia .
“Hivyo tuko hapa (Kampala ) kwa ajili ya
kufunga, ni lazima tufunge ili tuweze
kuendelea na mashindano . Lakini ngome
yetu nayo ni lazima iwe makini ili
kutoruhusu bao,” amesema Kim na
kuongeza kuwa kikosi chake cha kwanza ni
lazima kitakuwa mabadiliko kutoka na
Mwinyi Kazimoto kuingia mitini na Shomari
Kapombe kwenda kwenye majaribio
Uholanzi.
Amesema angalau kutakuwa na mabadiliko
kwa kuingiza sura mbili mpya katika kikosi
cha kwanza, na kuongeza kuwa wachezaji
wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo
kwani timu ikienda kwenye Fainali za CHAN
itakuwa manufaa kwao binafsi .
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager imefanya mazoezi ya
mwisho leo jioni Uwanja wa Mandela
ulioko Namboole ambao utatumika kwa
ajili ya mechi hiyo kesho.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni kwa
saa za Afrika Mashariki na itachezeshwa na
waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa
na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi
msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy
Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba
mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand
huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno
akiwa mwamuzi wa mezani ( fourth official).
Kamishna wa mechi hiyo namba 38 ni
Ismail Kamal kutoka Ethiopia.
Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende ,
Aggrey Morris , Kelvin Yondani , Athuman
Idd , Salum Abubakar , Frank Domayo , John
Bocco, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads