YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 5 Julai 2013

SH. 500/- SASA ITAKUWA SARAFU BADALA YA NOTI ILI KUIFANYA ISICHAKAE HARAKA

KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya
shilingi 500 na kiwango chake kudumu kwenye
mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), imesema inatarajia kubadili
noti hiyo na kuwa ya sarafu.
Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima juzi
kwenye viwanja vya maonesho ya kimataifa ya
biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa
Kitengo cha Fedha, Abdul Dollah, alisema
mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni
na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko
kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa na ubora
wake.
Dollah alitaja sababu nyingine ya uchakavu
huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na
watu wengi kwenye mzunguko huku baadhi
yao wakishindwa kuzihifadhi vizuri:

“Tofauti na noti nyingine kama vile zile za
sh 5,000 na 10,000 hizi utakuta mara
nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh
500 kwa sababu noti hizi watumiaji wake
wengi ni wale wenye akaunti benki.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads