YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 12 Julai 2013

"KILA MTANZANIA NI LAZIMA ALIPIE SH. 1000 KWA AJILI YA KADI YA SIMU YAKE"....WAZIRI WA FEDHA AMESISITIZA TENA

SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh
1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika
lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya
makato hayo kwa njia ambayo
haitamuumiza mtumiaji wa simu.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam,
Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa
alisema kuwa kupitia tozo hizo
wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa
mwaka.
“Kupitia wawakilishi wenu na sisi
serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na
ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa
kupata chanzo kingine cha mapato
kupitia kadi za simu” alisema.
Alisema katika mapendekezo yaliyokuwa
yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh
1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada
ya kukaa na kushauriana serikali iliona ni
vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi
aweze kumudu gharama ambapo kwa
mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu
atatozwa sh 12,000.
Alisema baadae serikali ilipokea
mapendekezo mbalimbali ili kuangalia
kama hilo linaweza kutekelezeka na
walipita ngazi zote kabla halijapelekwa
katika kamati za Bunge na kushauriwa
kwamba tozo hilo linaweza kufanyika kwa
lengo la kukuza uchumi hasa maeneo ya
vijijini.
“Tathmini zote zimefanyika kikamilifu
na baadae suala hilo likafikishwa
Bungeni ambapo pia napo lilikubalika...
inawezekana watu wanalalamika lakini
ngazi zote suala hilo lilipopita
lilikubalika na ikaonekana ni sawa
kutozwa sh 1,000 kwa kila kadi ya simu”
alisema.
Alisema kutokana na hilo kwa kutwa
nzima kadi ya simu itatozwa Sh 33.35 au
Sh 100 kwa siku tatu ambapo serikali
inaangalia utaratibu mzuri ambao
hautamuumiza mtumiaji wa simu.
Dk Mgimwa alisema fedha hizo
zitakazokusanywa zitaongeza upatikanaji
wa maji vijijini, umeme pamoja na
kuboresha miundombinu katika maeneo ya
vijijini.

Source: Habari Leo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads