YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumapili, 14 Julai 2013

BILIONEA WA MAREKANI AINUNUA FULHAM

Bilionea wa kimarekani , Shahid Khan
anayemiliki timu ya NFL ya Marekani
amenunua timu ya Fulham inayoshiriki
ligi kuu ya England . (HM)
TAJIRI Mohamed Al Fayed amethibitisha
kuiuza klabu ya Fulham kwa bilionea wa
Kimarekani, Shahid Khan , ambaye tayari
anamiliki timu ya NFL, Jacksonville Jaguars.
Uhamishwaji umethibitishwa na Ligi Kuu ya
England. Khan anamiliki asilimia 100 ya
hisa za klabu sasa na hakuna deni . Tangazo
rasmi lilitarajiwa kutolewa saa 7 jana
Craven Cottage.
"Wakati wa kuwa mmiliki wa Fulham
Football Club siku moja utafika mwisho, na
nafikiri wakati huo sasa umefika, "alisema
Al Fayed.
"Wakati ni mwafaka kwa sababu
nimempata mtu mzuri sana wa kuichukua ,
Shahid Khan amekubali kupokea majukumu
na kipaumbele ambacho nimekuwa nacho
Fulham tangu mwaka 1997 .
"Fulham itakuwa katika mikono mizuri
sana na Shahid , ambaye ni mfanyabiashara
mwenye mafanikio na mwenye mapenzi na
michezo kwa kila ushahidi . Naomba kila
mmoja anayependa Fulham na Uwanja
wetu wa nyumbani wa Craven Cottage
kumkaribisha Shahid kuanza safari yake ya
kuwa mlezi mpya wa Fulham Football
Club, "alisema.
Khan alisema: " Nimekuwa mwenye
bahati sana hivi karibuni , kutambulishwa
na Mohamed Al Fayed, mtu
ninayemuheshimu na kumzimikia kwa
mambo aliyoyafanya katika maisha yake na
- juu ya yote , kwa aliyowafanyia wengine, "

Chanzo: Globalpublishers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads