YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumamosi, 6 Julai 2013

BAADA YA SERIKALI KUPITISHA SHERIA YA KILA LAINI YA SIMU KULIPIWA SHILINGI 1,000 KWA MWEZI., MH. ZITTO KABWE AFUNGUKA...!!

Maneno haya yameandikwa na Mh. Zitto
Kabwe, jana tarehe 4 Julai kupitia akaunti yake
ya Facebook:
“Kodi ya Tshs 1,000 kwa mwezi Kwa kila kadi
ya simu uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la
wananchi, wawakilishi wa wananchi,
limepitisha kodi hii. Hailipwi na kampuni ya
simu, inalipwa na Wewe mwenye simu.
Kampuni ya simu inakusanya Kwa niaba ya
serikali. Ingawa sikuwepo wakati kodi hii
inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu
wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili. Ni
aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii
liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye
hotuba yake ya makadirio ya mapato ya
Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani
kupitia muswada wa fedha, finance bill,
Haieleweki. Ni skandali. Nasikia vibaya sana
kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi
ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba
hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo
hili.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads