Iliyopachikwa hapo chini ni video ya
Profesa Ibrahiumu H.
Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi (CUF) katika Msikiti wa Idrissa,
Kariakoo, jijini Dar es Salaam,
alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa,
miezi kadhaa iliyopita.
Prof. Lipumba alikaribishwa kuzungumza
na waumini hao mara baada ya utangulizi
uliotolewa na Imamu wa msikiti huo,
Sheikh Ali Basaleh, aliyemtaka awaeleze
Waislamu hali ya kisiasa nchini kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Baadhi ya nukuu: “Ninyi masheikh
mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa
ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike
juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi.
Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali
halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna
matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo
katika mtihani mgumu zaidi...”
“...wenzetu wameanza kujipanga, kwa
hiyo kama Waislamu tunataka kupata
haki zetu, kama tunataka kuishi kama
raia wa daraja la kwanza katika nchi
yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi
mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga
kwa sababu wenzetu wameanza
kujipanga, vinginevyo tutaendelea
kubaki maskini na raia wa daraja la nne
katika nchi yetu wenyewe."
http://www.youtube.com/watch?v=ujwfFUUAD70&feature=youtube_gdata_player
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni