YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 27 Mei 2013

Tokeo la kidato Cha "Nne na Sita" laweza tangazwa wiki hii:habari kamili bila chenga Soma hapa!

Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa
kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa
kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho
alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi
limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema
matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango
cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya
54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii
pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia
yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema
matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa,
ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne
umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa
matokeo yaliyotangazwa awali na huenda
yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba
watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali
walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya
awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya
ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka
2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa
mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126
sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya
mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema
upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado
unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa
mchakato unaendelea na matokeo
yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze
kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato
cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya
watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa
kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa
wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu
walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4.
Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327
sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909
sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu
ambayo imebadilika katika matokeo mapya
ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata
daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema
kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa
waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya
kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi
ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu
ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki
iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu
ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo
ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa
wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara
ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi
ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida
isingewezekana mtoto ambaye matokeo
yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie
ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa
upya baada ya wadau kuyalalamikia na
kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23,
mwaka huu.
Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake,
ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza
kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo
kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya
kukokotoa matokeo bila kushauriana na
wadau.
Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba
imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru
yapangwe upya kwa kufuata madaraja
yaliyotumika mwaka 2011.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads