YoungConcious™

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumapili, 16 Julai 2017

Beyonce hatimaye apiga picha na pacha wake

Beyonce apiga picha na pacha wake
 Beyonce apiga picha na pacha wake 
Beyonce hatimaye amesambaza picha ya kwanza aliyopiga na watoto wake pacha kuadhimisha mwezi mmoja tangu wazaliwe.
Msanii huyo wa Marekani alithibitisha kwamba majina yao ni Sir Carter na Rumi ambayo yalitolewa katika uvumi baada yeye na mumwe kuyatumia kama nembo ya biashara.
Picha hiyo inamuoyesha mama huyo mwenye umri wa miaka 35 na pacha hao wakiwa ndani ya shiti la rangi ya zambarau huku yeye mwenye akiwa amevalia vazi la rangi ya buluu
.Ilipata watu milioni mbili walioipenda katika mtandao wa Instagram katika saa moja tu.
Beyonce aliandika: Sir Carter na Rumi wamefikisha mwezi mmoja leo huku akiweka emoji ya mikono ya maombi na mwanamke, mwanamume na watoto wawili.
Mbali na pacha hao ambao ni mvulana na msichana Beyonce na JAY-Z pia ni baba wa mtoto wa miaka mitano Blue Ivy.
Beyonce katika picha aliyotangaza uja uzito wake
Beyonce katika picha aliyotangaza uja uzito wake
 
Mtindo wa picha hiyo ambapo Beyonce amesimama katika bustani akiwa hana viatu mbele ya eneo lenye maua unafanana na picha aliyopiga akitangaza uja uzito wake katika mtandao huo.
Ulimwengu ulikuwa ukisubiri kwa hamu kuwaona watoto hao tangu vyombo vya habari viliporipoti kwamba mwimbaji huyo wa Lemonade alikuwa amejifungua mwezi uliopita.
Lakini hakuna kati yao aliyethibitisha pacha hao .
Babake Beyonce Martin Knowles alituma ujumbe katika Twitter tarehe 18 mwezi Juni akisema: Ndio hawa 'happy birthday kwa pacha hao''- lakini wakati wa chapisho hilo la Beyonce linaonyesha kuwa watoto hao walizaliwa tarehe 14 mwezi Juni.
Haishangazi kwamba mashabiki walilazimika kusambaza maoni yao katika picha hiyo.
DJ wa BBC radio One Clara Amfo aliandika katika Twitter: Soo extra and I love it.

SOURCE: BBCSwahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads