YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 21 Aprili 2014

Fahamu TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLEVA WALIO INGIZA MSHIKO ZAIDI 2013.



TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLEVA  WALIO INGIZA MSHIKO ZAIDI 2013.

Muziki wa bongo fleva umezidi kutanua wigo wake nakuwa mpana hii imesababishwa na uelewa wa watu kujua kuwa muziki umekuwa ni ajira ambayo imekuwa iki wanufaisha vijana wengi.Na wasanii wenye hits,conection,majina wameendelea kujiingizia kipato kikubwa kutokana na muziki wao. hii ni list ya wasanii walio fanikiwa kuingiza pato kubwa kwa mwaka huu wa 2013 na hii nikutokana na shows,matangazona mauzo ya kazi zao.

#1. Diamond Platinum.
Bila ya ubishi kwa hakika Diamond kwa mwaka huu ndo aliye ingiza mkwaja mrefu zaidi na hii nikutokana na shoo zake za nje na ndani zilizo sababisha kuvuta mkwanja si chini ya Bilioni 1.
Kwa shoo za ndazni pekee diamond hutoza si chini ya milioni kumi mpaka 15,Na kila wiki hufanya shoo si chini ya mbili, hivyo tangu mwaka uanze Diamond amekua kila wiki akiingiza 40mil,Tour za nje alizo fanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya shoo kwenye miji mitatu, Shoo za burundi na congo,shoo mbili za kenya , show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000$. Kwa upande wa shoo za nyumbani alifanya shoo nyingi zisizo na idadi haswa za kill tour ambazo ndio alikuwa anaongoza kulipwa mkwanja mrefu kupita wote.

Pia kafanya shoo za fiesta, Shoo za promotion za tigo,tamasha la matumaini show, Tulizana tuko wangapi show,na nyingine nyingi.
Mkatabampya alioingia na kampuni ya vodacom yakuuza muito wa simu wa single yake mpya ya my no1 ndio ulizidi kumpandisha juu.
pia Diamond ni Balozi wa cocacola japo mkataba huo haujajulikana umemuingizia shilingi ngapi ila inasemekana sio chini ya milioni 100.


#2. Lady Jay dee.

Vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jide situ kujikusanyia mashabiki wengi bali hata kumuingizia kipato kikubwa sana zaidi ya tiketi 3500 zili nunuliwa katika shoo yake ya miaka 13 ya muziki na kuingiza sio chini ya milioni 100, Pia album yake ya Nothing but the truth imekuwa ikifanya vizuri sokoni hiyo kusababisha awe msanii pekee anayenufaika na mauzo ya album yake hapa Tz.
Hits zake mbili za Joto hasira na YAHAYA zimebadilisha maisha yake kumfanya kupata shoo nyingi zikiwemo za nje,ametumbuiza kwenye kill music tour zote ambapo ameingiza sio chini Ya mil 20.

Kitu kingine cha pekee ni shoo yake ya diary ya Jide ambayo ina dhaminiwa na air tell ambayo pia inamuingizia kipato.

#3. AY.

Humsikii sana rapa huyu kwenye shoo za Tz ila pesa zake nyingi zinatokana na biashara zake anazozifanya.Pesa nyingi alizoingiza zinatokana na ubalozi wa mwaka mmoja alioingia na Air tell.Katika mkataba huo Ay alilipwa dola zakimarekani 80,000 ambazo ni zaidi ya milioni 129.Pia rapa huyo ni balozi wa bia ya PERONI ya Italy na mkataba huo umemuingizia pesa nyingisana.Pia rapa huyo ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha Mkasi kinacho endeshwa na salama jabiri ambacho kina wadhamini wawili cocacola na Airtel kupitia mgawo huo wa mapato Ay amekuwa akidaka mshiko wakutosha.
Ay ni CEO wa kampuni ya Unity intertainment inayo jihusisha na uandaaji wa shoo kubwa mbalimbali kupitia kampuni hii imemwingizia pato kubwa sana Ay.
Kutokana na ukimya wa Rapa huyu nakutojionyesha ndo kitu pekee kinacho mfanya asijulikane kama ana ingiza paesa nyingi.

#4.Ommy Dimpoz
Ziara zake pekee za Ulaya na Marekani zimemuingizia zaidi ya milioni 80 zaki Tanzania.Tangu aachie wimbo wake mpya wa Tupogo tayari amesha ingiza milioni 50.Kwenye shoo yake ya hivi karibuni ya Tupogo night omy alipeleka sh.10mil hii ni baada ya makato yote  kwani walihudhuria watu takriban 1,770,kwa sasa anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye thamani ya mil250 mpaka zilipofikia.

#5.Madee.
Hii inaweza kuwashangaza wengi lakini madee amewaonyesha kuwa hata wimbo m1 unaweza ukakubadilisha kwa muda mfupi tu.Tangu atoe single yake ya sio mimi madee amesha ingiza si chini ya milioni 200.
Mwaka huu ameshafanya shoo za kampenia ya tigo 10 nakila moja akilipwa sh.3ml ,show 15 za airtel kwa kiwango hicho hicho napia alifanya shoo za cocacola zero zilizo mfanya aingize hela nyingi.

#6.Mwana FA.

Shoo yake ya the finest ilimuingizia mil19,Na hivi karibuni alichukuliwa na kampuni ya vodacom kuzunguka mikoani katika kampeni ya CCBRT kuhusiana na kukuza uelewa juu ya tatizo la fistula na kulipwa mkwanja mrefu kutokana na kampeni hizo.Mwana Fa amefanya matangazo kadhaa na vodacom na pia hivi karibuni aliingia mkataba na kampuni ya SUMSANG GALAXY kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo.
Amefanya show nyingi za nje kama kenya na South Africa ikiwa ni pamoja na za hapa ndani zikiwemo za Promotion.

#7.Chege.

Mwaka huu chege peke yake alifanya shoo 6 nje ambazo kila shoo alilipwa sh.4ml milioni nne, akiwa na Temba ambao kwa pamoja hutoza sh milioni 6.Chege amefanya shoo zaidi ya 30 zikiwemo za fiesta pamoja na promosheni mbalimbali.

#8.Prf.Jay
Prof.Jay aliingiza mil20 za kill music tour ,pia show kubwa na Jose chamilion wa Uganda, show kibao za promotion za makampuni show ya kampun ya IPP kwa ajili ya walemavu,na show nyingine za kawaida za Dar na mikoani.
pia amejikita katika biashara za saloon ambayo ianafanya vizuri,Na pia ameshafungua studio ya kurekodi mziki ambayo iko kwenye hatua za mwisho za kuanza kazi.

#9.Nay wa Mitego.
Tangu mwaka uanze Nay amesha fanya show zaidi ya 20 ambazo zimemwingizia si chini ya mil60,show hizo ni pamoja na show 2 za muziki gani,show za promosheni za makampuni ya simu,show za kil musik tour ,za fiesta na pia anabiashara zake ambazo kila mwezi humwingizia sio chini ya mil.4.
#10.Temba.
Fedha nyingi alizo ingiza ni kutokana na shoo walizofanya pamoja na chege ukitoa muziki,temba pia ni mfanya biashara anamiliki duka la vifaa vya ujenzi ambalo huwa lina muingizia si chini ya mil3 kwa mwezi.
Mwisho.
Endelea kutembelea blog hii Ndani ya wiki hii tutakupa Top10 ya wanamuziki wanaoongoza kwa utajiri Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads